Taarifa iliyotolewa leo January 05 2017 na Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia kwa msemaji wake Mindi Kasiga imesema kwamba Waziri wa mambo ya nje wa jamhuri ya watu wa China, Wang Yi anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini January 09 2017.
Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza mahusiano mazuri na ya kihstoria baina ya China Tanzania ambayo yamedumu kwa zaidi ya miaka hamsini tangu kuanzishwa kwake pamoja na kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na China.
Wakati wa ziara hiyo Wang Yi atakutana na Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa lengo la kumsalimia, aidha atafanya mazungumzo rasmi na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga.
Masuala ambayo yanategemea kuzungumzwa na viongozi hawa wawili
- Mpango wa uendelezaji wa viwanda ambapo inatarajiwa viwanda takribani 200 vinatarajia kujengwa au kuwekezwa nchini kutoka China kabla ya mwaka 2020
- Maboresho makubwa ya reli ya TAZARA
- Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo
- Ujenzi wa reli ya kati
- Masuala ya amani na usalama katika eneo la Afrika Mashariki pamoja na eneo la bahari ya kusini mwa China
VIDEO: Maamuzi mapya ya Waziri Mwigulu kuhusu mauaji ya wakulima na wafugaji, Bonyeza play hapa chini