Taarifa za kushikiliwa kwa rubani wa Kitanzania Mohamed Nassor na waasi nchini Sudan kusini zilisambaa December 28 mwaka jana zikieleza alikuwa akishikiliwa na waasi wa SPLM-IO ambapo imeripotiwa na baadhi ya vyombo ya habari kuwa alishikiliwa na waasi baada ya ndege aliyokuwa anaendesha kutua eneo ambalo wanalishikilia kiutawala.
Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki, kikanda na kimataifa imeeleza kuwa rubani huyo ameachiwa huru bila masharti yoyote ambapo msemaji wa wizara hiyo Mindi Kasiga ameeleza wamethibitisha kuachiwa kwake. Bonyeza play hapa chini kumsikiliza akifafanua….
VIDEO: Ufafanuzi kuhusu Watanzania waliokamatwa Malawi wakidaiwa ni majasusi, Bonyeza play hapa chini