Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com.
Moja ya habari kubwa iliyoandikwa na magazeti ya leo Jan 06 2017 ni pamoja na hii ya wafugaji 50 kuponea chupuchupu kufa kwenye pori la akiba la Selous.
#HabariLEO Wafugaji 50 chupuchupu kufa, walilanguliwa wakaingizwa pori la Selous na kutelekezwa, siku 7 wakila kinyesi cha ng'ombe, mkojo pic.twitter.com/D2SrxH0O8v
— millardayo (@millardayo) January 6, 2017
Gazeti la Habari leo limeripoti kuwa watu 50 wakiwa na watoto wamenusurika kufa baada ya kupotea ndani ya pori la akiba la Selous kwa siku saba, huku wakikosa chakula na maji na kulazimika kula kinyesi cha ngo’mbe, damu na mikojo ya binadamu.
watu hao ni wafugaji walikuwa wakihama na mifugo yao inayokadiriwa kufikia 1,780 kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Rufiji mkoani Pwani yakiwemo Chumvi na Muhoro wakielekea Morogoro ambako wanadai ndiko kuna makazi yao.
Wafugaji hao wanasema walitembea kwa siku tano ndani ya pori hilo, wakitarajia kufika Malinyi, yaliko makazi yao lakini hali ilikuwa tofauti, baada ya mwenyeji wao kuwalaghai kwa kuwapitisha njia zisizo sahihi.
Wanasema waliishiwa chakula na maji ya akiba na mwisho walijikuta wanatokea pori la akiba la Selous; huku hali zao zikiwa zimedhoofu kutokana na njaa na kiu cha maji, pale walipoishiwa chakula na maji iliwalazimu kuanza kuchinja ng’ombe na kunywa damu kwa ajili ya kukata kiu pia walikula kinyesi cha ng’ombe ili kupunguza njaa.
Yule mwenyeji wao aliwatelekeza baada ya kuona hali zao zimekuwa mbaya, alitokomea kusikojulikana, akiwaacha wasijue pa kwenda, hivyo kulazimika kutelekeza mifugo yao ili kunusuru kwanza maisha yao.
Kiongozi wao anasema baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya alitafuta eneo lenye mtandao wa simu na kufanya mawasiliano mbalimbali na kuomba msaada.
#HabariLEO Wafugaji 50 chupuchupu kufa, walilanguliwa wakaingizwa pori la Selous na kutelekezwa, siku 7 wakila kinyesi cha ng'ombe, mkojo pic.twitter.com/D2SrxH0O8v
— millardayo (@millardayo) January 6, 2017
#NIPASHE Baadhi ya walimu Shinyanga wadaiwa kutoroka vipindi darasani na kuingia kwenye biashara ya bodaboda na kupiga picha mitaani pic.twitter.com/ItJaW1JqrP
— millardayo (@millardayo) January 6, 2017
#MWANANCHI DAS Monduli, Siyantemi ashauri utafiti ufanyike kuona uwezekano wa kutumia damu za wanyama kuwaongezea binadamu wenye upungufu pic.twitter.com/ASQd6tclTr
— millardayo (@millardayo) January 6, 2017
#MTANZANIA 'Kama mvua haijanyesha hadi leo ni lazima tuchukue tahadhari'-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pic.twitter.com/9qrYxl6qhb
— millardayo (@millardayo) January 6, 2017
#JamboLEO Mmoja wa wakurugenzi watatu TANESCO walioshushwa vyeo, Decklan Mhaiki asema yuko tayari kufanya kazi kokote ndani ya shirika hilo pic.twitter.com/kng99iJbpH
— millardayo (@millardayo) January 6, 2017
#UHURU Serikali imeliagiza jeshi la zimamoto na uokoaji na uhamiaji kukitumia kiwanda cha ushonaji cha magereza, kutengeneza sare za askari pic.twitter.com/lnZjm7SXWn
— millardayo (@millardayo) January 6, 2017
#UHURU K'ndoni kuokoa Bil 4 mwaka huu wa fedha kwa kutengeneza mfumo kwa kushirikiana na TAKUKURU ili kudhibiti wizi wa dawa vituo vya afya pic.twitter.com/bR88gdunkx
— millardayo (@millardayo) January 6, 2017
#TanzaniaDAIMA GK awataka wasanii nchini kutafuta elimu nje ya muziki ili siku mambo yakienda vibaya wawe na uwezo wa kufanya mambo mengine pic.twitter.com/2oHtAtkQZo
— millardayo (@millardayo) January 6, 2017
#HabariLEO Viwanda takribani 200 vinatarajiwa kuwekezwa nchini na Serikali ya China kabla ya mwaka 2020 pic.twitter.com/Iev0FkztDd
— millardayo (@millardayo) January 6, 2017
#MWANANCHI Waziri Mkuu Majaliwa asisitiza utunzaji wa chakula kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyosababisha mvua kuchelewa pic.twitter.com/PY8yaNbZnW
— millardayo (@millardayo) January 6, 2017
#MWANANCHI Daktari asema watumiaji wa bodaboda hatarini kuambukizwa maradhi ya ngozi kutokana na matuimzi ya kofia ngumu 'helmeti' chafu pic.twitter.com/LhTFFQBlwa
— millardayo (@millardayo) January 6, 2017
AyoTVMAGAZETI: Panga kufyeka wengine TANESCO, Sababu tatu za ukame wanafunzi shule binafsi, Bonyeza play hapa chini