Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com.
Moja ya habari iliyoandikwa leo January 10 2017 ni pamoja na hii ya gazeti la Mwananchi yenye kichwa cha habari Polisi washtukia mbinu mpya ya ‘wauza unga’
#MWANANCHI Imeelezwa 'Wauza unga huingiza nchini kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kifua kisha kuvitumia kutengeneza Cocaine, Heroin pic.twitter.com/jfMpA9eQp5
— millardayo (@millardayo) January 10, 2017
Gazeti la Mwananchi limeripoti kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamebuni mbinu mpya kwa kusafirisha na kuingiza nchini, vibashirifu (kemikali zinazotumika kutengeneza dawa ya kifua) aina ya ephedrine kisha kuvitumia kutengeneza cocaine na Heroin.
Kamanda wa polisi, kikosi cha dawa za kulevya, Mihayo Msikhela amesema kwamba wafanyabiashara hao usafirisha kemikali hizo kutoka bara la Asia na wanapozifikisha nchini hutumia kutengeneza dawa hizo za kulevya.
Kadhalika amesema wafanyabiashara hao hununua kemikali hizo bila kuwa na kibali cha serikali na hudanganya na hudanganya kuwa zitatumika kutengeneza dawa za kifua.
Nimekuwekea hapa nyingine 10 kubwa zilizoandikwa na magazeti ya Tanzania leo January 10 2017
#NIPASHE Imeelezwa kuwa mpango wa serikali wa kukopa kwenye benki za biashara za ndani utarudisha fedha iliyoadimika mitaani kwa sasa pic.twitter.com/3y3xXae63V
— millardayo (@millardayo) January 10, 2017
#NIPASHE Trump akubali Russia ilijihusisha na udukuzi wa mtandao wa kompyuta wakati wa uchaguzi wa urais wa Marekani pic.twitter.com/kzwxNFft1Y
— millardayo (@millardayo) January 10, 2017
#UHURU Baadhi ya wanawake nchini walio ktk umri wa kuzaa lakini hawazai wapo ktk hatari ya kupata uvimbe 'fibroids' kwenye mfuko wa uzazi pic.twitter.com/6i0o1Y3V9o
— millardayo (@millardayo) January 10, 2017
#HabariLEO Mama mzazi wa mtoto wa miezi minane na mganga wa kienyeji mbaroni kwa mauaji ya mtoto kwa lengo la kujipatia utajiri Simiyu pic.twitter.com/M1o6zoqpGu
— millardayo (@millardayo) January 10, 2017
#HabariLEO Askari wa TANAPA Manyara watuhumiwa kumpiga na kisha kumgonga kwa gari mkazi wa Monduli kwa tuhuma za kukamatwa na nyama ya twiga pic.twitter.com/KofKmPfFBJ
— millardayo (@millardayo) January 10, 2017
#HabariLEO Polisi Igunga imewakamata watu watatu wakiwa na noti bandia za sh 10,000 zipatazo mia nane sawa na sh milioni nane pic.twitter.com/f1kSFz2H6N
— millardayo (@millardayo) January 10, 2017
#JamboLEO Rais Obama amemshauri mrithi wake Trump kuwa asijaribu kuendesha Ikulu kama anavyoongoza familia yake au anavyofanya biashara pic.twitter.com/AeJRQtdo2T
— millardayo (@millardayo) January 10, 2017
#MTANZANIA Imeelezwa maeneo mengi ya nchi yamekumbwa na njaa ambayo imesababisha na kukosekana mvua muda mrefu pic.twitter.com/tKyTmSmipl
— millardayo (@millardayo) January 10, 2017
#TanzaniaDAIMA Mashabiki wa muziki nchini Kenya wamemtaka Darassa kwenda haraka Kenya kufanya show pic.twitter.com/FgRlcp0LOk
— millardayo (@millardayo) January 10, 2017
#MTANZANIA Watu zaidi ya 200 wamekamatwa ktk kipindi cha mwaka jana kutokana na makosa ya kukutwa na nyara mbalimbali za serikali pic.twitter.com/bk4B3kuC8E
— millardayo (@millardayo) January 10, 2017
AyoTVMAGAZETI: Hatimaye fedha kurudi mtaani, Serikali yashtuka ubia na shule za masingi, Bonyeza play hapa chini
Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE