Kumekuwa na tatizo la uhaba wa damu salama katika vituo vya matibabu nchini jambo ambalo limepelekea wengine kushauri utafiti wa kisayansi ufanyike ili kuona uwezekano wa kutumia damu za wanyama kwa ajili ya kuwekewa binadamu wenye uhitaji huo.
AyoTV na millardayo.com imempata Dkt Heri Tungaraza kulizungumia hilo, Dkt Tungaraza amesema …..
>>>Tafiti zinaendelea kufanyika dunia nzima kuona ni mnyama gani tunaweza tukamtumia, wanyama ambao wako karibu na sisi ni sokwe, tatizo wako wangapi duniani, hawa ni kati ya wanyama ambao wako hatarini kumalizika dunia nzima’
>>>’Damu zao hata kama zinafanana na sisi, bado hazifanani kwa asimilia ambayo wanaweza kutupa sisi hiyo damu na madhara yoyote kutojitokeza’
VIDEO: Prof. Maji marefu baada ya kutembelewa na waziri Mkuu hospitali, Bonyeza play hapa chini kutazama