Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com.
Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo ni pamoja na hii ya kwenye gazeti la Habari leo yenye kichwa cha habari ‘Amjeruhi vibaya mwanawe kwa kumtahiri kwa kisu’
Gazeti hilo limeripoti kuwa mkazi wa kijiji cha Mihingo wilayani Bunda mkoani Mara, Marwa Elias amefikishwa mahakama ya wilaya ya Bunda kwa tuhuma ya kumtahiri vibaya kwa kutumia kisu, kukata kipande kikubwa cha uume wa mtoto na kumsababishia madhara makubwa mwilini mwake.
Kwa sasa mtoto anajisaidia haja ndogo kwa shida kutokana na kukatwa sehemu hiyo ya siri vibaya. Inadaiwa baada ya tendo hilo mtuhumiwa huyo alitoweka na kwenda kwenye shughuli zake akimuacha mtoto huyo akiwa kwenye hali hiyo, baadaye hivi karibuni alikamatwa na kufikishwa polisi na kisha mahakamani.
Baada ya kusomewa shtaka lake mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na kupelekwa mahabusu katika gereza la Nyasura nje kidogo ya mji wa Bunda, baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Unaweza kuzipitia hapa chini habari nyingine kubwa zilizoandikwa
#HabariLEO Manusura wasimulia ajali ya jahazi Tanga, wasema upepo uliipiga ikakatika, miili 12 yapatikana, ilikuwa na abiria zaidi ya 50 pic.twitter.com/AgcARsLz83
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#HabariLEO Bodi ya utendaji ya shirika la fedha duniani 'IMF' imeeleza kuwa hali ya uchumi wa Tanzania ni nzuri pic.twitter.com/9l6J28pOFD
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#HabariLEO Serikali imezindua kifaa kipya cha kugundua ugonjwa wa selimundu ambacho kitatoa majibu ndani ya dakika tano pic.twitter.com/BAUelR0XyY
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#HabariLEO Jeshi la Polisi Tarime Mara linawashikilia watu 10 kwa udhalilishaji wa kumchapa viboko mwanamke hadharani pic.twitter.com/tmIFYbqW14
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#HabariLEO Afikishwa mahakama ya wilaya ya Bunda kwa tuhuma za kumtahiri vibaya mwanawe kwa kutumia kisu, kukata kipande kikubwa cha uume pic.twitter.com/KRPPv74Fqf
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#MWANANCHI Mtandao wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya umebainika kuwepo katika kituo kikuu cha mabasi Mbeya pic.twitter.com/N0ALO7mHMN
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#MWANANCHI Mkazi wa Manyara auawa kwa kipigo kisha kutolewa utumbo, mtu alilipwa kufanya mauaji, inadaiwa ili wagawane mali za marehemu pic.twitter.com/vvjicy9iqK
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#MWANANCHI Familia za wasichana 80 waliokimbia kukeketwa Tarime zadaiwa kukataa kuwapokea baada ya kituo kilichokuwa kikiwatunza kuvunjwa pic.twitter.com/A6GxRc5Un1
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#NIPASHE Wakazi wa kijiji cha Kibamba kata ya Mipeko, Mkuranga mkoani Pwani, hawana zahanati tangu kijiji hicho kianzishwe mwaka 1974 pic.twitter.com/rHAPirjSkB
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#NIPASHE Mnada wa ng'ombe wadorora Mvomero Morogoro, wafugaji wahofia kukamatwa na polisi baada ya wenzao mnada wa Dumila kukamatwa pic.twitter.com/aiRbx2NlDx
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#NIPASHE TRA mkoa wa Morogoro imeshika nafasi ya pili kwa makusanyo 2015/16 kwa kukusanya bil 56.9 na kuvuka lengo la kukusanya bil 50.58 pic.twitter.com/VzEVboQ0Sr
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#NIPASHE Wabunge wa chama cha Democrat wataka maamuzi ya Trump kumteua mkwe wake kuwa mshauri mkuu upitiwe kwa hofu ya kuwepo upendeleo pic.twitter.com/Vd5XGbibuG
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#MTANZANIA Imeelezwa kuwa maofisa polisi wawili wamechukuliwa hatua kutokana na kushindwa kushughulikia tukio la mauaji ya watafiti Dodoma pic.twitter.com/oxmqxlS3CC
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#MTANZANIA Wafanyakazi waliofukuzwa kwa kukosa sifa hospitali ya Ifisi Mbeya wameilaumu Serikali kuwaacha wenzao 21 walioghushi vyeti pic.twitter.com/VVovsNrUbu
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#MTANZANIA Rais Magufuli anatarajiwa kuadhimisha siku ya mapinduzi ya Z'bar ktk uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga pic.twitter.com/MP1ayRjtpu
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#MTANZANIA Imeelezwa kuwa ujenzi holela unaozidi kukua kwa kasi mkoani Arusha ni miongoni mwa changamoto kubwa inayokabili sekta ya ardhi pic.twitter.com/XBgNDpEusU
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#MTANZANIA Idadi ya mauzo ktk soko la hisa la DSM imepanda kwa 59% kutoka bil 8.3 hadi kufikia bil 13.2 pic.twitter.com/0e14OIsdRA
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#JamboLEO Askofu kanisa la Anglikana DSM, Dk. Valentino Mokiwa amesema mgogoro ktk kanisa hilo ni wa kutengenezwa na hauna uhalisia pic.twitter.com/ynFG2PArHQ
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#JamboLEO Vyama vya upinzani nchini Kenya kutangaza mgombea mmoja wa urais mwezi ujao, ikiwa ni miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu pic.twitter.com/SXpInDvdti
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#JamboLEO Idadi kubwa ya wanaume wanofika hospitali ya KCMC Moshi kupima saratani ya tezidume hugundulika kuathirika kwa kiwango kikubwa pic.twitter.com/hgSVjf3QSd
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
#JamboLEO Bohari ya dawa 'MSD' imesema upatikanaji wa dawa nchini unatarajiwa kuwa kati 86% hadi 90% kwa January hadi March pic.twitter.com/rVSDBbXNqn
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
AyoTVMAGAZETI: IMF yaeleza hali ya uchumi waTZ, Manusura wasimulia ajali ya Jahazi Tanga
Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE