Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com.
Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo ni pamoja na hii ya kwenye gazeti la Nipashe, yenye kichwa cha habari ‘Gereza aliko mbunge CHADEMA labainishwa’
#NIPASHE Imefahamika kuwa mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali yupo ktk gereza la Ukonga DSM baada ya kifungo cha miezi sita jela pic.twitter.com/tQgiUk3gW1
— millardayo (@millardayo) January 19, 2017
Gazeti hilo limeripoti kuwa Mbunge wa Jimbo la Kilombero mkoani Morogoro kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo ‘CHADEMA’, Peter Lijualikali yupo katika gereza la Ukonga jijini Dar es salaam baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela.
Jumatano iliyopita, mahakama ya wilaya ya Kilombero ilimhukumu kumikia kifungo cha miezi sita jela bila kulipa faini mbunge huyo kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki.
Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza na Gazeti la Nipashe jana kwa simu, alisema alimtembelea mbunge huyo kwenye gereza la Ukonga alikofungwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Unaweza kupitia hapa chini nyingine kubwa 10 kutoka kwenye magazeti ya leo
#JAMBOLEO Wabunge sita kutoka mikoa ya Kusini waunda umoja ili kuibana Serikali kuhusu majibu ya suluhu ya migogoro ya wakulima na wafugaji pic.twitter.com/iLPpQUpQzH
— millardayo (@millardayo) January 19, 2017
#BINGWA Mshambuliaji wa kimataifa Emmanuel Okwi sasa njia yake kurejea Simba ni nyeupe baada ya kuvunja mkataba na club yake ya Sonderjyske pic.twitter.com/rdYBtqn1xm
— millardayo (@millardayo) January 19, 2017
#NIPASHE Imeelezwa kuwa mgodi wa madini ya dhahabu wa Buzwagi Kahama kufungwa miezi 11 kuanzia sasa kwa kuwa madini yatakuwa yameisha pic.twitter.com/hgM2B6ewuD
— millardayo (@millardayo) January 19, 2017
#MTANZANIA Watu waishio karibu na barabara kuu wapo hatarini kupata matatizo ya afya ya akili, yapo ya kupoteza kumbukumbu, kubadili tabia pic.twitter.com/yN219LuTBt
— millardayo (@millardayo) January 19, 2017
#NIPASHE Baadhi ya wafanyabiashara wanaotafutwa kwa kutorosha makontena 329 wamebadili majina ya biashara zao ili kukwepa kukamatwa pic.twitter.com/oc43u7BUre
— millardayo (@millardayo) January 19, 2017
#MTANZANIA Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis aahidi kufanya mageuzi ktk mfumo wa mahakama, kesi zitasajiliwa kielekitroniki ili kuwa wazi pic.twitter.com/ekFDscFMIU
— millardayo (@millardayo) January 19, 2017
#NIPASHE Wanasayansi Uingereza wagundua utaalamu wa kupima mkojo wa mwanadamu na kugundua kila alichokula kwa mchanganuo wake kamili pic.twitter.com/LdxDB6gqs5
— millardayo (@millardayo) January 19, 2017
#NIPASHE Watafiti wamesema bangi ni chanzo cha vijana kujinyonga na kuacha shule pic.twitter.com/LwZoIVECmJ
— millardayo (@millardayo) January 19, 2017
#MTANZANIA Nauli za ndege Air Tanzania Dar-Mwanza 160,000, Dar-Arusha 160,000, Dar-Bukoba-Dar 499,000, Dar-Mbeya-Dar 265,000, Dar-ZNZ 80,000 pic.twitter.com/FKIwW4FWvs
— millardayo (@millardayo) January 19, 2017
#MTANZANIA Wananchi mkoani Tanga wapata matumaini mapya ya kupata mvua baada ya Kakakuona kufanya utabiri kuhusu kuanza kwa mvua kubwa pic.twitter.com/ZKp2HiArtb
— millardayo (@millardayo) January 19, 2017
AyoTVMAGAZETI Viongozi watatu wa Chadema wafungwa, Ujenzi wa hospitali wamng’oa kigogo, Bonyeza play hapa chini