Mix

Maneno ya Freeman Mbowe kuhusu viongozi wawili wa CHADEMA waliohukumiwa miezi 8 jela

on

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe akiwa Mwanza amezungumzia ishu ya viongozi wawili wa chama hicho ambao wamehukumiwa kwenda jela miezi 8 kwa kosa la kufanya mikutano ya hadhara bila kibali.

Mbowe amewaambia Waandishi wa habari Mwanza >>> ‘Tumepata taarifa za kusikitisha kwamba Mwenyekiti wetu wa chama wa mkoa wa Lindi pamoja na katibu wa kijiji kimoja wapo kule, Suleiman Mathew amehukumiwa kwenda jela kwa miezi 8 bila faini

Utakumbuka ni wiki iliyopita tu Mbunge wetu wa Kilombero nae amehukumiwa kwenda jela miezi 6 bila faini, wanahukumiwa kwenda jela bila faini kwenye makosa ambayo kimsingi yanayo adhabu za faini kwa nia ya kuwakomoa‘ – Mbowe

Kutazama alichosema Freeman Mbowe unaweza kukipata hapa chini kwenye hii video

VIDEO: Tazama hapa chini David Kafulila alivyokabidhiwa rasmi kadi yake ya CHADEMA 

Soma na hizi

Tupia Comments