Wanasema Arusha ni mji wa wagumu na ndio maana una sifa ya kuwa na Wasanii wengi wanaofanya Hiphop lakini ugumu huo usiutegemee kwenye ndoa, Wanaume wa Arusha mwaka 2016 wameshindwa kuvumilia na kuripoti zaidi wanavyonyanyaswa na Wake zao kuliko miaka ya nyuma.
Makao makuu ya Kitengo cha Dawati la Jinsia Arusha kupitia kwa Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu yametoa taarifa ambapo Happyness ameongea na AyoTV na millardayo.com na kusema mwaka 2016 matukio ya Wanaume kunyanyaswa Arusha idadi iliongezeka karibu mara mbili ikilinganishwa na ya mwaka 2015.
Anasema ‘kumekua na ukatili wa kijinsia na wengi wanadhani ukatili huu wanafanyiwa Wanawake peke yake lakini ukweli ni kwamba wapo Wanaume wanaonyanyaswa pia na sasa hivi wameamka kuliko zamani‘
‘Wanaume wanaofanyiwa ukatili ikiwemo kunyimwa tendo la ndoa ni wengi, huwa wanakuja kulalamika… idadi ya Wanaume waliokuja mwaka 2016 imepanda kutoka 34 mwaka 2015 na kufikia 63 mwaka 2016 ambayo ni sawa na asilimia 48‘ – Happyness
BONGO MOVIE: Mume kaenda kazini…… Wife kaleta Mchepuko nyumbani