Siku moja kabla ya kumalizika kwa michuano ya AFCON 2017 kwa kuchezwa mchezo wa fainali kati ya Misri na Cameroon, usiku wa February 4 ulichezwa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya timu ya taifa ya Burkinafaso dhidi ya timu ya taifa ya Ghana.
Ghana ambao walitolewa katika hatua ya nusu fainali ya AFCON 2017 kwa kufungwa na Cameroon 2-0, wamejikuta wakipokea kipigo cha pili mfululizo baada ya Burkinafaso kufanikiwa kupata goli la ushindi dakika ya 89 kupitia kwa Abdou Razak Traore na kuifanya Ghana kuikosa nafasi ya tatu ya michuano ya AFCON 2017.
Mchezo wa Ghana na Burkinafaso ulikuwa ni mchezo ambao takwimu zake ziko kwa karibu, kwani baada ya mchezo wa leo Ghana na Burkinafaso wanakuwa wamekutana kwa mara ya 17 wakiwa wamewahi kutoka sare mechi moja na kila timu ikimfunga mwenzake mara 8.
Baada ya mchezo huo Jumapili ya Februay 5 2017 itakuwa ni zamu ya kumfahamu Bingwa mpya wa michuano ya AFCON 2017 kati ya Cameroon dhidi ya Misri, fainali hii inajirudia fainali ya AFCON 2008 ambapo Misri aliifunga Cameroon kwa goli 1-0 na kutwaa taji lake la sita la AFCON, wakati huo goli lilifungwa na Mohamed Aboutrika.
https://youtu.be/UW_kkjCHXSI
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4