Wekeend iliyopita taarifa kutokea Mwanza zilisema kuwa baadhi wananchi na Machinga wanaofanyabiashara kwenye eneo la Buhongwa waliwatupia mawe askari Mgambo na kusababishia majereha kwa baadhi ya askari.
Jeshi la Polisi Mwanza linawashikilia watu kadhaa wanaodaiwa kushiriki kwenye tukio hilo, Sasa AyoTV na millardayo.com imetafuta Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula kuhusu tukio hilo na kitendo cha yeye kutokuhudhuria vikao vya halmashauri.
“Nilichofanya ni kumtaarifu mmoja wa viongozi wanaosimamia operesheni hii na kumwambia watu wanaoitwa mgambo na hawako kwenye mavazi rasmi ya mgambo wamevamia na shughuli wanayoifanya sasa hivi si ya kuondoa watu kwa kuwa zoezi la kuondoa watu walishalifanya jana ilikuwa wameenda kufanya shughuli nyingine kabisa”
Waziri Nape alivyokutana na Wamiliki wa Vyombo vya habari TZ