Agizo la Rais Dk. John Magufuli la kutaka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ‘TPDC‘ kukamilisha makubaliano na kampuni ya Dangote Group of Industries juu ya bei ya mauziano ya gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya kiwanda hicho cha kutengeneza saruji kilichopo Mtwara limetekelezwa.
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi mtendaji wa TPDC, Kapuulya Musomba amesema wamekubaliana juu ya kuunganishwa miundombinu ya kusafirisha gesi asilia kutoka kwenye bomba kubwa la gesi kwenda kwenye kiwanda cha Dangote pamoja na kukamilisha mkataba wa awali kwa ajili ya mauziano ya gesi kwa matumizi ya kiwanda hicho. Unaweza kubonyeza play hapa chini kutazama
VIDEO: Makamu wa Rais Samia Hassan alivyozindua utoaji wa ‘IPAD’ kwa wanafunzi Dodoma, Bonyeza play hapa chini kutazama