Wanasayansi nchini Australia wamegundua matumizi ya sumu ya Buibui katika kuukinga ubongo usiharibiwe kutokana na kiharusi.
Watafiti nchini Australia walifanya uchunguzi wa vinasaba (DNA) katika sumu ya Buibui na kugundua chembechembe ambazo wanasema zinaweza kuzikinga seli za ubongo hata kama zitatumika saa kadhaa baada ya mtu kupata kiharusi.
“Tunaamini kwamba, kwa mara ya kwanza, tumegundua njia ya kupunguza athari za kuharibika kwa ubongo baada ya kiharusi,” – Professor Glenn King wa UQ Institute for Molecular Bioscience.
Wanasayansi wa University of Queensland na Monash University walifanya ugunduzi huo walipochunguza sumu ya Buibui ambayo inaweza kuua binadamu ndani ya dakika 15 lakini wamegundua protein ya Hi1 ambayo siyo sumu na inaweza kutumika kama mbadala wa kutibu kiharusi.
VIDEO: Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye alipozungumza kinachoendelea kuhusu Makonda. Bonyeza play hapo chini kutazama.