Leo March 27, 2017 millardayo.com inakusogezea hii ambayo huko kwenye mji wa Chongqing China ambao ukitaka kusafiri huhitaji kuufuta usafiri bali usafiri unakufuata mpaka eneo la nyumbani kwako.
Mji wa Chongqing uliopo kusini-mashariki mwa China imeusogeza karibu na wakazi wake usafiri wa treni kwa reli kupita kwenye baadhi ya nyumba za kuishi watu pia kuna vituo ambavyo wakazi wa eneo hilo husubiri usafiri huo.
Mji huo pia unafahamika kama ‘Mountain City’ una wakazi wapatao 49 million, hivyo kuwafanya wasanifu majengo na maafisa wa mipango miji kubuni njia hiyo kurahisisha usafiri.
AyoTV MAGAZETI: Ulikosa kujua kilichoandikwa kwenye magazeti ya Tanzania March 26, 2017? Bonyeza play kutazama.