April 6, 2017 millardayo.com inakusogezea story ambayo inahusu Roboti iliyotengenezwa kwa mfano wa Pweza ambayo imekamilika na huenda ikaanza kufanya kazi sanjari na binadamu hivi karibuni.
Robot hiyo inaitwa OctopusGripper na imebuniwa na Kampuni ya maroboti ya Festo ya Ujerumani na kutengenezwa kwa mfano wa kiumbe wa baharini mwenye miguu minane na misuli laini inayomuwezesha kujikunja kwa namna awezavyo na itafanya kazi kwa salama na binadamu.
“Pweza ni kiumbe wa ajabu. Hana gofu la mifupa (skeleton) na ameumbwa kwa misuli laini, pia anaweza kujikunja awezavyo. Hii haimaanishi kuwa anaweza kuogelea pekee kwenye uelekeo wowote, lakini pia kwa namna anavyoweza kukamata kitu chochote. OctopusGripper sasa imeyachukua mambo yote.” – Festo.
Bonyeza play hapo chini kutazama namna OctopusGripper inavyofanya kazi…
https://youtu.be/ZPUvA98uSj8
VIDEO: Kama ulikosa kuwaona Serengeti Boys walipoanza safari ya AFCON U-17 Gabon April 5, 2017. Bonyeza play kutazama.