Kufuatia agizo la serikali lililotolewa na mkuu wa mkoa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu,juu ya wafugaji kuondoa mifugo yao katika mapori ya akiba na misitu ya hifadhi mkoani humo imepelekea operation ya kuwaondoa kwa nguvu kuanza kutekelezwa.
Kaimu mkurugenzi huduma za ulinzi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) Faustine Masalu amesema kuwa tangu March 30 mwaka huu operation hiyo ilianza rasmi ambayo itadumu kwa siku kumi na nne ambapo kufikia leo jumla ya mifugo 1,922 imekamatwa na watuhumiwa 19 wakiwemo Watanzania 14, warundi watatu na wanyarwanda wawili.
Watuhumiwa hao wote kwa pamoja watafikishwa Mahakamani kesho April 3, 2017. Full stori unaipata kwenye hii video hapa chini…
VIDEO: Mtoto mwenywe uwezo wa kujibu maswali papo kwa papo kataja timu na viongozi
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo