Baada ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kushuka mfululizo katika viwango vya soka dunia vinavyolewa kila baada ya mwisho wa mwezi na FIFA, leo April 6 2017 Tanzania imepokea good news kutoka FIFA baada ya kupanda katika viwango hivyo.
Kwa kawaida viwango vya FIFA hupangwa na shirikisho la soka duniani FIFA kila mwezi kwa kuangalia matokeo ya mechi za kimataifa zilizochezwa na zinazotambuliwa na FIFA katika mwezi husika, Tanzania kwa sasa imefanikiwa kusogea hadi nafasi ya 135 kutoka nafasi ya 157 yaani imepanda kwa nafasi 22.
Katika kipindi cha mwezi March Tanzania imecheza mechi mbili dhidi ya Burundi iliyoshinda kwa goli 2-1 dhidi ya Botswana iliyoshinda kwa goli 2-0, Tanzania wakati inacheza na Burundi ilikuwa nafasi ya 139 na imeshuka hadi nafasi ya 141 wakati Botswana ilikuwa 116 na imeshuka hadi 120.
ALL GOALS: Taifa Stars vs Botswana March 25 2017, Full Time 2-0