Muimbaji staa wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda ameingia kwenye headlines baada ya kushutumiwa kumtaka kimapenzi mke wa msanii mwenzake wa Bongo Fleva Bamuyu.
Kupitia U-heard ya XXL leo April 7 Bamuyu amedai kuwa Nuh anamvunjia heshima kwa kumtumia sms na kumpigia simu akimtaka mke wake.
Soudy Borwn aliwatafuta wawili hao kujua ukweli na majibu yao yalikuwa haya…>>>“Nuh ananikosea heshima. Na tumefikia huko maana amekuwa mara kwa mara anamsumbua mke wangu, anampigia simu na kumtumia massage akiwa anamtaka ndiyo maana nikaona nimkanye. Ninachoweza kumwambia ni kitu kimoja, namfuata hadi kwao.” – Bamuyu.
>>>”Bamuyu ndiyo nani? Mimi simjui na simfahamu, na sielewi unachoniambia. Kwanza mniache mimi na mke wangu na familia yangu. Mbona mnaniandama sana? Hebu kidogo wasikilize wimbo wa shishi ‘Hatutoi kiki’ na kama anakuja, aje tu kama wimbo wa Alikiba.” – Nuh Mziwanda.
Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full story…
VIDEO: ‘Nilipata zero Kidato cha Nne, haimaanishi kuwa sina akili’ – Nuh Mziwanda