Rais Magufuli, leo April 10, 2017 ameteua wajumbe wa Kamati maalumu ya pili itakayofanya uchunguzi wa kiwango cha madini yaliyomo kwenye mchanga kwenye makontena yaliyozuiliwa kusafirishwa nje ya nchi yakiwa maeneo mbalimbali nchini.
Kamati hiyo yenye wajumbe 8 inajumuisha Wachumi na Wanasheria imetanguliwa na Kamati ya kwanza iliyoundwa na wataalamu wa masuala ya Jiolojia, Kemikali na Uchambuzi wa Kisayansi.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa ni;
⦁ Prof. Nehemiah Eliachim Osoro
⦁ Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara
⦁ Dkt. Oswald Joseph Mashindano
⦁ Bw. Gabriel Pascal Malata
⦁ Bw. Casmir Sumba Kyuki
⦁ Bi. Butamo Kasuka Philip
⦁ Bw. Usaje Benard Usubisye
⦁ Bw. Andrew Wilson Massawe
Wajumbe hao wataapishwa na Rais Magufuli April 11, 2017 saa 3:00 Asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.
VIDEO: Rais Magufuli alivyokutana na kuzungumza na Balozi wa Umoja wa Ulaya IKULU. Bonyeza play kutazama.