Ni wazi inafahamika kuwa amani na usalama ni msingi katika maisha ya binadam ambapo bila kuwa na amani na usalama hakuna kinachoweza kufanyika, hivyo uwepo wa amani mahali popote kunapelekea mambo mengi kufanikiwa.
Leo April 12, 2017 nimekutana na stori ambayo inaihusu World Economic Forum kutoa list ya nchi zenye usalama zaidi duniani ambapo katika taarifa iliyochapishwa na mtandao wa The Telegraph April 11, 2017 nchi ya Finland imetajwa kuwa namba moja kwa kuwa na usalama zaidi duniani huku nchi zenye historia ya vita kama Rwanda, Oman na United Arab Emirate zikiingia kwenye Top Ten ya mwaka 2017.
Aidha, katika list hiyo pia zimetajwa nchi zisizo na usalama duniani ambapo barani Afrika nchi za Kenya, Ethopia, DR Congo na Mali zimetajwa kama nchi zenye viashiria vya vurugu na zisizo na usalama ambapo kwa mujibu wa World Economic Forum, nchi hizi hupata watalii wachache kwa mwaka ukilinganisha na nchi nyingine.
VIDEO: Ulipitwa na hii ya Rais Magufuli kukabidhiwa ripoti ya TAKUKURU? Bonyeza play kutazama.
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo