Nahodha wa timu ya taifa ya England na club ya Man United Wayne Rooney leo April 12 2017 ameandikwa na mtandao wa express.co.uk kuwa ameamua kuwaeleza wachezaji wenzake wa Man United kuwa ataondoka Man United mwisho wa msimu.
Wayne Rooney katika msimu wake huu wa mwisho wa Man United amekuwa akikosa nafasi kubwa ya kucheza chini ya kocha Jose Mourinho lakini mwezi February aliripotiwa kuhitajika na vilabu vya Chinese Super League.
Rooney mwenye rekodi ya ufungaji katika club ya Man United amekuwa akipata nafasi ndogo ya kucheza Man United tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma hivyo anajiandaa kwenda kucheza sehemu nyingine kutokana na kutokuwa na uhakika wa namba kwa siku za usoni.
Wakala wa staa huyo Paul Stretford amekuwa akiitafakari dili ya staa huyo kwenda kucheza China au Marekani lakini timu yake ya zamani ya Everton inamuhitaji na kama atakubali atalazimika mshahara wake kupunguzwa kwa pound 100,000.
VIDEO: Simba imekubali kipigo cha nne cha VPL vs Kagera April 2 2017