Baada ya taarifa za kuuawa kwa askari polisi wanane eneo la Kibiti, mkoani Pwani kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika, leo April 14 2017 Jeshi la Polisi Makao Makuu limekutana na wanahabari kutolea ufafanuzi sakata hilo.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Nsato Marijani amesema askari waliouawa walikuwa wanatoka kubadilisha lindo ndipo wakashambuliwa kwa risasi katika barabara ya DSM-Lindi na kusema sasa Jeshi hilo linaingia kwenye oparesheni maalum ya kuwatafuta majambazi hao.
'Kuanzia sasa jeshi la polisi linakwenda kwenye oparesheni maalumu hatutokuwa na mzaha wala msamaha'-Nsato Marijani pic.twitter.com/Naytv9A5do
— millardayo (@millardayo) April 14, 2017