April 21, 2017 ni siku ambayo ilikuwa na matukio mbalimbali ndani na nje ya Tanzania katika nyanja za siasa, uchumi, utamaduni na jamii ambapo moja ya stori inayo-make headline kwa Afrika Mashariki inaihusu Kenya.
Unaambiwa kampuni ya China Road & Bridge Corporation (CRBC) ya China imesema Reli ya Standard Gauge kutoka mji wa Mombasa hadi jiji la Nairobi nchini Kenya ambayo itakuwa ya kwanza nchi humo itazinduliwa May 31, 2017.
Mahakama Kuu nchini Urusi imekubali ombi la serikali la kufuta kundi la Mashahidi wa Yehova na kulitaja kama kundi lenye msimamo mkali #BBC pic.twitter.com/L8AvATpoHP
— millardayo (@millardayo) April 21, 2017
Utafiti uliofanywa nchini Ufaransa umebaini kuwa dawa za kifafa zinaweza kuathiri afya za watoto wachanga, hasa kwa wanaotarajia kujifungua pic.twitter.com/3TrKD4f7Qe
— millardayo (@millardayo) April 21, 2017
Benki ya dunia imesema kasi ya ukuaji wa uchumi barani Afrika inaridhisha mwaka huu tofauti na mwaka 2016 ambapo uchumi ulizorota kwa kasi pic.twitter.com/LDBRhx9omE
— millardayo (@millardayo) April 21, 2017
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewaonya watu wanaopanga kufanya njama za kuvuruga Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika August mwaka huu. pic.twitter.com/GReACJ5GTf
— millardayo (@millardayo) April 21, 2017
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Kgalema Motlanthe amesema hana uhakika kama atamuunga mkono Rais Jaco Zuma na ANC katika Uchaguzi Mkuu ujao pic.twitter.com/meZNyMuFZc
— millardayo (@millardayo) April 21, 2017
Wagombea 11 wa Urais nchini Ufaransa wamewasilisha mikakati yao kwenye mdahalo wa mwisho wa televisheni kabla ya Uchaguzi Mkuu April 23,2017 pic.twitter.com/mb63KfJ4iA
— millardayo (@millardayo) April 21, 2017
China Road & Bridge Corporation (CRBC) ya China imesema Reli ya Standard Gauge Mombasa-Nairobi ya kwanza nchi humo itazinduliwa May 31, 2017 pic.twitter.com/SoYWtroANM
— millardayo (@millardayo) April 21, 2017
Watu 7 wamefariki na wengine kujeruhiwa baada ya kupigwa shoti ya umeme wakitazama mechi ya Manchester United na Anderlecht nchini Nigeria pic.twitter.com/L3DptMOSSE
— millardayo (@millardayo) April 21, 2017
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amekutana na mwakilishi wa WHO nchini, Dr. Matheau Kamwa anayechukua nafasi ya Dr. Rufaro Chotara aliyehamia S.A pic.twitter.com/CPq7ylp5Ci
— millardayo (@millardayo) April 21, 2017
Taasisi ya Elimu nchini Kenya imesema Wizara ya Elimu inakamilisha mchakato wa kuongeza lugha ya Kichina kwenye mtaala wa masomo nchini humo pic.twitter.com/kqh5CiSwB1
— millardayo (@millardayo) April 21, 2017
VIDEO: Malori 600, madereva na matingo 1,200 wa Tanzania wamezuiliwa Zambia. Bonyeza play kutazama.