Saa kadhaa baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kuamua kumshitaki mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara katika kamati ya maadili ya TFF kufuatia maneno yake aliyoyatoa wakati akizungumza na waandishi wa habari April 19, Simba imetangaza mpango wao mpya.
Baada ya TFF kufikia maamuzi hayo na kuweka wazi kupitia vyombo vya habari, Rais wa wekundundu wa Msimbazi Simba Evans Aveva ameamua kuandika barua ya kuomba kibali cha kufanya maandamano ya amani kutokea makao makuu ya Simba Kariakoo hadi wizara ya michezo siku ya Jumanne ya April 25.
Simba wanafikia maamuzi hayo ya kupeleka malalamiko yao kwa waziri habari, sanaa, utamaduni na michezo kwa kile wanachoamini kuwa hawatendewi haki na TFF, hivyo ni vyema kwenda kuomba msaada katika wizara husika wakiamini ufumbuzi wa malalamika yao utatatuliwa kwa haki na usawa.
Simba wameomba kufanya maandamano ya amani April 25 kuanzia Msimbazi hadi kwa waziri wa michezo kupeleka malalamiko yao #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/VrPpfqjTak
— millard ayo (@millardayo) April 21, 2017
VIDEO: Msimamo wa Simba uliyotolewa leo kuhusu point 3 vs Kagera Sugar