Bado wachezaji na benchi zima la ufundi la Man United halitakuamini kwa kilichotokea kwa mshambuliaji wao tegemeo raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic kuwa hawezi kurejea uwanjani kwa siku za karibuni kufuatia jeraha lake la goti alilolipata wakati wa game ya Europa League dhidi ya Anderletch.
Kwa mujibu wa mitandao ya Ulaya hususani ESPN umeripoti kuwa Zlatan Ibrahimovic kufuatia jeraha lake la goti la kulia alilolipata atakaa nje ya uwanja hadi mwezi January 2018, kitaalam Zlatan anaumwa Anterior Cruciate Ligament (ACL), hivyo atalazimika kufanyiwa upasuaji ambao utamchukua muda mrefu kurudi uwanjani.
Jeraha hilo alilolipata Zlatan mastaa wenzake ambao wamewahi kukutana na tatizo hilo wamekuwa wakikaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi 9, mfano Zouma wa Chelsea aliumia katika mchezo dhidi ya Man United 2016 lakini alilazimika kurudi uwanjani baada ya miezi 11.
Inawezekana huo ndio ukawa mwisho wa Zlatan kuvaa jezi ya Man United kutokana na mkataba wake kuripotiwa kumalizika mwisho wa msimu huu, sasa haijajulikana kama staa huyo aliongeza mkataba na Man United au alikuwa ameingia makubaliano ya awali kama hakuongeza ana asilimia ndogo ya kupewa mkataba mpya akiwa katika majeruhi na akiwa na miaka 35.
VIDEO: Msimamo wa Simba uliyotolewa leo kuhusu point 3 vs Kagera Sugar