Bado headlines za soka la bongo kwa sasa ni kuhusiana na mvutano unaoendelea baina ya club ya Simba dhidi ya shirikisho la soka Tanzania TFF, Simba wamekuwa wakiituhumu TFF kutowatendea haki kwa mambo kadhaa na kuamini kuwa TFF wanawapendelea wapinzania wao Yanga.
Simba wametangaza kufanya maandamano ya amani siku ya Jumanne ya April 25 kutoka makao makuu yao Kariakoo hadi wizara yenye dhamana ya michezo kupeleka malalamiko yao, kufuatia malalamiko hayo ya Simba, Baraza la Michezo Tanzania BMT kupita katibu mkuu wake Mohamed Kiganja wameagiza mambo matano yafanywe na TFF na Simba.
VIDEO: Msimamo wa Simba uliyotolewa leo kuhusu point 3 vs Kagera Sugar