Moja kati ya stori ambayo imechukua nafasi katika siku za hivi karibuni ni kuhusu Mtanzania ambaye ameanzisha nyumba maalumu kwa ajili ya kuwatibu vijana walioathirika na dawa za kulevya maarufu kama Sober House.
Ricky ni Mtanzania ambaye aliathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ambapo baada ya kutibiwa ameachana na matumizi ya dawa hizo na kuamua kuanzisha kituo chake cha kutibu na kuwapa ushauri watanzania wengine ambao wameathiriwa na dawa za kulevya kiitwacho South Beach Sober House kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam kikiwa na matawi sehemu mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaokoa vijana wengine ambao walikuwa watumiaji wa dawa hizo za kulevya.
Ayo TV na millardayo.com imepiga stori na Mkurugenzi wa South Beach Sober House, Ricky ambaye moja ya mambo aliyoyazungumzia ni pamoja na lengo la kuanzisha kituo hiko.
“Lengo na madhumuni ya kituo ni kusaidia ndugu zangu, jamii yangu, familia na mtu yeyote ambaye alikuwa anahisi ana tatizo la dawa za kulevya. Kituo kimeendelea kutoa huduma, tumepata mafanikio mengi sana kwa sababu kubwa ya mafanikio tuliyokuwa tunayatafuta, ndugu zetu wanarudi katika maisha, wanakuwa wanachama wazalishaji katika jamii.” – Ricky.
Bonyeza play kutazama…
VIDEO: Waathirika wa dawa za kulevya wapewa elimu ya ujasiriamali. Bonyeza play kutazama…