Duniani

Upasuaji wa kupandikiza kichwa unatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2017

on

December 2017 inatarajiwa kuwa siku ya kihistoria kwenye sekta ya afya na tiba duniani ambapo utafanyika upasuaji wa kupandikiza kichwa kwa mara ya kwanza utakaofanyika mjini London ikihusisha madaktari 150 na itachukua zaidi ya saa 34.

Kwa mujibu wa Daktari atakayeongoza upasuaji huo Dr. Sergio Canavero, upasuaji huo utafanyika kwa mara ya kwanza kwa binadamu ambapo kichwa cha binadamu aliye hai kitapandikizwa kwenye mwili wa mtu aliyekufa na binadamu huyo kuweza kupata mwili mpya.

Madhumuni ya upasuaji huu ni kusaidia watu waliopata magonjwa ya kupooza viungo, watu wenye vilema vya miguu na magonjwa ya uti wa mgongo kupata matumaini mapya ya kuwekewa mwili mwingine. Upasuaji huu unatajwa kugharimu zaidi ya Dollar millioni 30.

Upasuaji utafanywa kwa mara ya kwanza kwa mgonjwa Valery Spiridonov kutoka Urusi ambaye kitaondolewa kichwa chake na kupandikizwa kwenye mwili wa mtu aliyekufa. Valery Spiridonov amejitolea kufanyiwa upasuaji huou kwa sababu ana tatizo la uti wa mgongo liliopelekea mwili wake kupata ugonjwa wa kiharusi.

VIDEO:Ulipitwa na huu utafiti kuhusu dawa ya uzazi wa mpango ya panya kutumika kwa binadamu?Bonyeza play kutazama

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo 

 

Soma na hizi

Tupia Comments