Yapo mambo mengi sana yanayostaajabisha kutoka kila sehemu ya dunia hii, lakini mengine yanastaajabisha zaidi na kuvunja rekodi mbalimbali za dunia.
Katika hali ambayo pengine wengi huenda wasiamini kwa sababu haijazoeleka kutokea Afrika hasa katika nchi kama Tanzania ambapo ukiachilia mbali Mlima Kilimanjaro na Mbuga ya Serengeti ambazo zipo kwenye rekodi ya dunia, lakini ukweli upo kwamba mtu mwenye umri mkubwa zaidi anapatikana pia Tanzania.
Utakuwa umesikia rekodi ya binadamu mzee zaidi duniani ambaye anatokea katika nchi ya Jamaica Bi. Vailet Brown ambaye amezaliwa March 10, 1900 ambapo kwa sasa ana umri wa miaka 117 huku mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 97.
Ayo TV na millardayo.com inakuletea rekodi mpya kutoka Tanzania – nayo ni kuhusu mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani ambaye anaishi Mkoa mpya wa Songwe katika Wilaya ya Mbozi, Kata ya Ihanda, Kijiji cha Majengo.
Kutoka huko nakuletea Ambilikile Panja ambaye anakadiriwa kuwazaliwa mwaka 1890 ambapo kwa mwaka 2017 atakuwa ametimiza miaka 127 na kumzidi mtu anayetambuliwa na Guinness Book of World Records Vailet Brown kwa miaka 10.
Bonyeza play hapa chini kutazama…
VIDEO: “Inawezekana inatafsiriwa mimi ni mtu katili, wa ajabu” – Rais Magufuli. Bonyeza play kutazama…