Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘TAKUKURU’ Mkoa wa Temeke imezitaja taasisi ambazo zinaongoza kwa kulalamikiwa kwa vitendo vya rushwa ndani ya tisa iliyopita ikiongozwa na Halmashauri ya Temeke.
Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Temeke Pilly Mwakasege amezitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na Manispaa ya Temeke, Mahakama, sekta binafsi, Polisi, Ardhi, Afya na Idara nyingine.
Mpaka sasa TAKUKURU imefungua mashauri mapya matatu Mahakamani huku mashauri manne yakiwa yanaendelea kusikilizwa Mahakamani katika hatua mbalimbali huku ikiokoa zaidi ya Tsh. 99m ikiwemo mishahara hewa na kujilipa posho isiyo halali ndani ya miezi hiyo tisa.
Nimekuwekea hapa full video, bonyeza play kutazama…
VIDEO: Alichokisema Spika Ndugai wakati akizindua semina ya kupambana na Rushwa Dodoma. Bonyeza play kutazama…