February 27 2016 katika ukumbi wa Karimjee Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, Diwani wa Kata ya Kimanga, Manase Njema, mfanyabiashara na kada wa chama hicho, Rafii Juma na Diwani wa Kata ya Saranga Kimara, Ephreim Kinyafu walidaiwa kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando.
Leo May 4 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa maamuzi kuhusu kesi hiyo ambapo mahakama hiyo imewaachia huru wabunge hao baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu.
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha, hata mlalamikaji Mmbando hakumbuki ni nani aliyemjeruhi.
Aidha ameongeza ushahidi wake ulielezea Jinsi washtakiwa walivyojishughulisha na nyaraka siku ya tukio na siyo kumjeruhi, hivyo hakimu aliwaachia huru washtakiwa wote kwa kuwa hawana kesi ya kujibu.
VIDEO: Marufuku Magazeti kusomwa Redioni na TV Tanzania – Dr. Mwakyembe, Bonyeza play hapa chini