Siku moja baada ya kukamilisha usajili wa kuvidhamini vilabu vya Ligi Kuu Tanzania bara kwa kuidhamini Singida United baada ya Simba na Yanga, Sport Pesa leo kupitia Mkurugenzi wao Abbas Tarimba wametangaza kuanzisha mashindano ya Sport Pesa Super Cup.
1- Mashindano ya Sport Pesa Super Cup yataanza June 5 2017 na yatakuwa yakishirikisha timu nane kutoka Kenya na Tanzania zinazodhaminiwa na Sport Pesa.
2- Mashindano hayo yatafanyika kwa mfumo wa mtoano na yatafanyika kwa siku 12 pekee, kwa mwaka huu yatafanyika Tanzania na mwakani yatafanyika Kenya.
3- Kwa Tanzania timu nne zitashiriki ambazo ni Simba, Yanga, Singida United na Jang’ombe Boys wanaoongoza Ligi ya Zanzibar, wakati timu kutoka nje ya Tanzania zitakazoshiriki ni FC Leopard, Tusker FC, Nakulu All Stars na Gor Mahia.
4- Michezo yote itachezwa katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na mshindi wa michuano hiyo atapewa zawadi ya Tsh milioni 66 wakati mshindi wa pili atapewa zawadi ya dola 10000 ambazo ni zaidi ya Tsh Milioni 20.
5- Timu zote nane zitapewa Tsh milioni tano kama ada ya ushiriki na zitakazocheza hatua ya nusu fainali kila moja itapewa dola 5000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 10.
6-Marefa watakaokuwa wanachezesha game hizo sio kutoka Tanzania wala Kenya lengo ni kuepusha lawama za upande mmoja kuhisi unaonewa, marefa wa Tanzania watakuwepo pale lakini sio kama waamuzi wa kati.