Waziri wa Afya Ummy Mwalimu May 29, 2017 amekutana na Waandishi wa Habari DSM ambapo amezungumzia kuhusu ugonjwa wa EBOLA ambao umekuwa tishio katika nchi za Afrika akisema hakuna mtu aliyegundulika kuwa na ugonjwa huo hapa Tanzania.
Ili kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini Waziri Ummy amesema Serikali imeanza kusambaza vifaa maalum vya kupimia ugonjwa huo sehemu zote za mipaka ya nchi na Viwanja vyote vya Ndege Tanzania akiitaja pia Mikoa Tisa ambayo imetakiwa kuchukua hatua kukabiliana na Ebola.
Hivi karibuni Shirika la Afya Duniani WHO liliripoti kuwepo mlipuko wa EBOLA katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hasa katika jimbo linalopakana na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
VIDEO: Ulipitwa na hii stori ya watu watano kuhukumiwa kifo Kagera? Bonyeza playkutazama!!!