Jumatatu ya wiki iliyopita ulimwengu wa soka hususa barani Afrika ulipokea taarifa za kushusha kuhusiana na kifo cha kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast aliyekuwa anaichezea Beijing Enterprises ya Beijing China.
Tiote ambaye amewahi kuichezea timu ya Newcastle United ya England alifariki ghafla mazoezini akiwa na timu yake ya Beijing, ameagwa na wachezaji wenzake wa Beijing na leo June 14 mwili wake unasafirishwa hadi kwao Ivory Coast.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Cheick Tiote alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Ivory Coast waliyotwaa Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015, Tiote hadi anapoteza maisha alikuwa kacheza jumla ya mechi 246 ngazi ya club huku timu ya taifa ya Ivory Coast ameichezea michezo 52.
Cheick Ismael Tiote alizaliwa June 21 1986 Yamoussoukro Ivory Coast alianza safari yake ya kucheza soka mwaka 1998 katika club ya FC Bibo ya kwao Ivory wakati huo akiwa na umri wa miaka 12, mwaka 2008 akiwa na miaka 22 akajiunga na Anderlecht ya Ubelgiji.
Safari yake ya soka haikuwa rahisi na hata Anderlecht hakupata nafasi ya kucheza sana na akapelekwa kwa mkopo Roda JC, baadae akajiunga FC Twente na mwaka 2010 akajiunga na Newcastle United aliyoichezea kwa miaka sita na miezi kadhaa kabla ya mwaka 2017 kuamua kujiunga na Being Enteprises.
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera