Wakati Dunia ikisubiri kuadhimisha Siku ya Kupambana na Kuenea Hali ya Jangwa na Ukame Duniani June 17, 2017, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba leo June 16, 2017 amekutana na Waandishi wa Habari Dodoma kuelezea takwimu ya athari ilizozipata Tanzania kutokana na hali ya ukame…
Makamba amesema…>>>”Nchi yetu inakabiliwa kwa kiasi kikubwa na hali ya kuenea kwa jangwa na ukame. Takwimu zinaonyesha kuwa takriban asilimia sitini na moja (61) ya eneo la nchi liko katika hatari ya kugeuka jangwa“
“Miongoni mwa mikoa ambayo imeathirika zaidi ni pamoja na Singida, Dodoma, Shinyanga, Manyara, Simiyu, Geita na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Arusha” –Makamba
“Tayari madhara mbalimbali ya kuenea kwa hali ya jangwa na ukame yameanza kuonekana ikiwa ni pamoja na kukauka kwa vyanzo vya maji katika maeneo mbalimbali, vifo vya mifugo na wanyama pori, upungufu wa mvua kutokana na ukataji wa miti kiholela, migogoro baina ya wafugaji na wakulima kutokana na kupungua kwa maeneo ya kilimo na malisho ya mifugo” –Makamba
VIDEO: Alichoongea Mbunge Musukuma Bungeni kuhusu sakata la Madini