AyoTV na millardayo.com zilikua miongoni mwa vyombo vya habari vilivyoalikwa na Taasisi ya kupambana na rushwa TAKUKURU kwenye mkutano na Waandishi wa habari, ni mkutano ambao uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu Valentino Mlowola.
Alianza kwa kusema >>> ‘Tunataka kuwapa taarifa za mapambano yetu dhidi ya rushwa na ufisadi nchini…. na leo tunawapa taarifa kwamba tunawafikisha Mahakamani Watuhumiwa wawili ambao ni James Rugemalila na Harbinder Singh Sethi”
“Tunawafikisha Mahakamani kwa makosa ya uhujumu uchumi na makosa mengine yanayofanana na hayo, kwa muda mrefu sana nimekua naulizwa kesi za ESCROW na IPTL zimeishia wapi, kama tulivyosema mwanzo…. TAKUKURU ina jukumu la kimsingi la kupambana na rushwa na ufisadi”
“Tulichunguza shauri hili kwa muda mrefu na sasa umefika wakati muafaka wa kuwafikisha Watuhumiwa hawa wakuu Mahakamani, tayari wameshapelekwa Mahakamani” – Mlowola
Unaweza kutazama hii video hapa chini kwa taarifa kamili