Jeshi la Polisi DSM limekutana na Waandishi wa Habari na kutolea ufafanuzi mambo mbalimbali yaliyojiri na moja kati ya mambo hayo ni issue ya Walemavu waliotawanywa kwa mabomu ya machozi baada ya kuziba Barabara ya Sokoine June 16, 2017 wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa.
Naibu Kamishna wa Polisi ambaye pia ni Mkuu wa Operation za Kipolisi Kanda Maalumu ya DSM anayekaimu nafasi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya DSM Lucas Mkondya amesema:>>>”Hatujatumia nguvu ya kupita kiasi. Tumetumia nguvu kulingana na hali ya watu ambao walikuwa wanafanya maandamano hayo.
“Ulemavu, nataka nitoe rai kwa wananchi ulemavu sio kibali cha wewe kuvunja sheria wala ulemavu haukupi wewe kibali cha kuvunja sheria za nchi. Sheria za nchi zipo kwa mtu yeyote yule – mzima au mlemavu na hasa ambaye anazifunja kwa makusudi akijua.
“Hawa walemavu walifanya makosa, wamevamia Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa lakini pamoja na hivyo wakaziba njia. Tumejaribu kuongea nao kuwasihi kwamba wafungue njia lakini pia wateue viongozi wao kwenda kushughulikia matatizo yao lakini walikaidi. Kwa hiyo, ikabidi tutumie nguvu kidogo tukaenda kuwaondosha tukafungua barabara na wananchi wengine wakaendelea na shughuli zao.” – Kaimu Kamanda Lucas Mkondya.
TAKUKURU yatangaza watu wawili inaowapeleka Mahakamani