Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ‘LHRC’ kimekutana na Waandishi wa Habari DSM leo June 20, 2017 kutoa tamko lake baada ya Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya Walemavu ambao walifunga Barabara DSM June 16, 2017.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Anna Henga amesema kituo hicho kinalaani kwa nguvu zote kitendo cha Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kuwatawanya walemavu hao.
“Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi kwa Watu wenye Ulemavu tumesikitishwa na tunaalani vikali kitendo cha matumizi ya nguvu kubwa iliyopitiliza kilichofanywa na Jeshi la Polisi Tanzania katika zoezi la kuzuia maandamano ya watu wenye ulemavu tarehe 16, 6 2017 eneo la Posta Jijini Dar es Salaam.
“Kundi la watu wenye ulemavu ni moja kati ya makundi maalumu katika Jamii yetu linalohitaji na kuwekewa ulinzi kwa mujibu wa Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mikataba ya kikanda na kimataifa bado wanastahili heshima na utu wao kama binadamu wengine.
“Kwa hivyo basi, kitendo cha kuwapiga, kuwaburuza na kuwadhalilisha na kuwaharibia nyenzo wanazotumia kutembea ama kusapoti shughuli zao za kila siku ni matumizi mabaya ya ngumu ya Mamlaka dhidi ya kundi hilo yanayohatarisha usalama wa watu wenye ulemavu.” – Anna Henga.
Msimamo wa ACT Wazalendo baada ya Walemavu kupigwa mabomu DSM