Dec 2013 hii ndege inayotajwa kuwa ya Ethiopia ilitua kwa dharura kwenye kiwanja cha ndege Arusha (87.9 Clouds FM) ambacho kitaalamu hakiwezi kuhimili kupokea ndege kubwa kama hii ndio maana hata ilivyotua ilipitiliza mpaka kwenye majani na hapo unaambiwa rubani alicheza kwelikweli.
Anyway, ninachotaka kuzugumzia kwenye hii post ni jinsi ambavyo watu mbalimbali walijitokeza kuishangaa hii ndege tena siku ya kwanza na ya piliambapowalikaa kwenye eneo la tukio kwa saa kadhaa bila shughuli maalum, yani walikua wanashangaa tu na kutaka kujua nini kitatokea.
Picha zote hizi unazoziona nilizipiga siku ya pili baada ya kwenda kwenye eneo la tukio ambapo kwa harakaharaka nilivyohesabu idadi ya magari yaliyokua yamepaki ndani ya dakika 11, ni magari 26 huku watu wakiwa mamia kwenye pande zote mbili za barabara iliyokua pia na foleni kiasi kwenye eneo hilo.
Kwa siku za karibuni Watanzania mbalimbali wamekua wakitoa maoni kwenye millardayo.com pamoja na page zangu za facebook, twitter na instagram/millardayo kuhusu tabia ya wengi wetu kukusanyika kwenye tukio bila kuwa na shughuli maalum ya kufanya bali kushangaa tu.
Tukio lililowakasirisha wengi ni la Sinza Shekilango January 2014 ambako kifaa kinachofanana na bomu kilionekana lakini cha kushangaza baada ya kelele kupigwa na kusambaa kwa taarifa za bomu, watu walikusanyika haraka sana kwenye eneo la tukio kushuhudia na sio kukaa mbali kwa hofu ya mlipuko.