Bado siku zinahesabika kufikia July 13 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ambapo tutaona kikosi cha kwanza cha Everton ya England kikicheza game ya kirafiki na Bingwa wa SportPesa Super Cup timu ya Gor Mahia ya Kenya.
Timu ya Everton itawasili Dar es Salaam July 12 siku moja kabla ya game lakini msafara wao wa kwanza utafika Dar es Salaam July 8, inawezekana hujui faida itakazozipata Tanzania kwa ujio Everton kwa mara ya kwanza katika historia ya club hiyo ambayo haijawahi kushuka daraja toka EPL ianzishwe 1992.
Mkurugenzi wa utawala na utekeleza wa SportPesa Tanzania Abbas Tarimba amezungumzia faida Tanzania itakazozipata “Tukiacha dakika 90 za game ya Gor Mahia na Everton, Tanzania itafaidika sana na ujio huo kwa mfano kutangaza Everton inakuja Tanzania tayari ukiingia mitandaoni ukitafuta utakuta habari nyingi zinaandikwa na mitandao mbalimbali duniani kuhusu Tanzania”
“Tanzania itazidi kusemwa vizuri na itazidi kutengeneza uaminifu kwa watu wa nje kuwa Tanzania ni sehemu salama kutembelea lakini sio kutembea peke yake inaweza pia kuvutia uwekezaji kwa maana, wachezaji 25 wa Everton thamani yake ukiipiga kuja Tanzania watu watajiuliza kuna nini Tanzania hadi Everton waende? hivyo inaongeza shauku ya watu kuja”
VIDEO: Good News nyingine kwa soka la Bongo kutoka SportPesa