Leo June 25, 2017 mengi yameripotiwa kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania kuhusu siasa, uchumi, utamaduni na jamii yakiandikwa kwenye Magazeti na kutangazwa kwenye Televisheni na Radio na mitandaoni.
Kama hukusikia kuhusu hatma ya waliokata rufaa baada ya kukutwa na vyeti feki, kitisho cha magonjwa ya mlipuko na ongezeko la vitendo vya uhalifu basi time yako ni hii kuyajua mambo hayo kupitia millardayo.com ambayo imekukusanyia mambo yote hayo na kukusogezea karibu.
Serikali imesema watumishi wa umma waliokutwa na vyeti feki kisha kukata rufaa hatma yao itajulikana mwishoni mwa mwezi huu. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Mfanyabiashara Yusuf Manji amemuomba radhi Rais JPM kutokana na mvutano wake na Serikali kuhusu umiliki wa ufukwe wa Coco DSM. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Wakulima wadogo wa mazao mbalimbali Mkoa wa Lindi wameshauriwa kutunza mavuno na kuepuka madalali ili kupiga hatua kiuchumi. #NIPASHE.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
CHADEMA Bunda imesema kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu wilayani humo huchangiwa na kutokuwepo kwa wenyeviti wa vitongoji. #NIPASHE.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Z'bar imetakiwa kuwa makini ktk kutafuta haki kwa kuwa rushwa hurudisha nyuma maendeleo. #NIPASHE
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Wamiliki wa nyumba, makazi na viwanda wamefikishwa ktk Baraza la Ardhi na Nyumba Tanga wakishindwa kulipa kwa wakati kodi ya 1.1b. #NIPASHE.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Washiriki wa Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba wametakiwa kujifunza kutoka kwa washiriki wengine wa kimataifa. #NIPASHE.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka DSM (DAWASA), Mhandisi Archad Mutalemwa ameanza likizo ya kustaafu. #NIPASHE.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Wachimbaji wadogo 1,000 Shinyanga wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko hasa kipindupindu kutokana na ukosefu wa vyoo. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Serikali inaangalia uwezekano kuondoa gharama za utoaji huduma (service charge) ambazo watumiaji hutozwa bila hata kutumia maji. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Zanzibar imesema haitanunua karafuu kutoka Bara kuingia soko la Zanzibar kwa kuwa imepata ithibati na kutambuliwa kimataifa. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
RC Ruvuma amewaagiza viongozi wote mkoani humo kudhibiti matumizi ya pombe iliyofungwa kwenye mifuko ya plastic 'viroba'. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Serikali mkoani Mbeya imesisitiza kuwa itapiga chapa mifugo yote iliyopo mkoani humo ili kudhibiti uingizwaji holela wa mifugo. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Serikali imesema mgawo kwa wawekezaji walioomba kununua hisa katika masoko ya mitaji utatoa kipaumbele kwa watanzania. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Kampuni za mafuta na gesi zimetakiwa kununua huduma na bidhaa zilizopo nchini ili kwenda na mahitaji ya sheria ya mafuta ya 2015. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Serikali imeanza kufanya maboresho ya mfumo wa usajili na kuanzisha mfumo utakaofanyakazi vizuri kusajili matukio muhimu. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA) kimeiomba Serikali kuingilia kati uharakishwaji wa madai ya mirathi kwa wajane. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Zaidi ya 50% ya mapato ya kodi yanayokusanywa kila mwaka kwenye nchi za Afrika ikiwemo Tanzania hupotea kutokana na rushwa. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewataka wanaodaiwa na bodi hiyo kulipa ili wengine nao wakope.#TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) June 25, 2017
Diamond Platnumz kaongea baada ya Rayvanny kushinda Tuzo ya BET