Story kubwa ambayo inatrend kwenye mitandao mbalimbali kuanzia kwenye Televisheni, Radio, mitandao ya Kijamii na Magazeti leo June 27, 2017 ni kuhusu aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuitwa na DCI kuhojia.
Pamoja na hayo lakini yapo pia mengine kuhusu issue ya maiuaji yanayoendelea Kibiti, Rufiji na Mkuranga pamoja na nasaha zilizotolewa kwenye Baraza la Eid el Fitr ambayo kwa pamoja nimekukusanyia na utayapata hapa millardayo.com.
Halmashauri ya Bunda, Mara imezindua Jukwaa la Wanawake kwa lengo la kuwakutanisha Wanawake wote kujadili fursa na changamoto. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
DC Bagamoyo amewataka wananchi kuhakikisha wanaenzi na kutekeleza mema yote waliyoyatenda wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya Iringa Blaston Gaville amemuomba Rais JPM kumazilia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Wanawake wilayani Kondoa, Dodoma wametakiwa kuacha tabia ya kujifungulia majumbani ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Viongozi wametakiwa kusaidia Taifa kukemea mavazi yanayoshawishi ngono yanayovaliwa na wanavyuo ambayo humdhalilisha pia mwanamke #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Watoto wanaoishi katika mahabusu ya watoto Arusha wameomba msaada kwa wanasheria kuwasaidia katika kesi zao mbalimbali. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Wananchi na Watumishi wa Umma Visiwani Zanzibar wametakiwa kutimiza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa juhudi ili kufikia malengo. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry amehimiza umoja, upendo na mshikamano kwa Waislamu na Watanzania ili kulinda amani. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Imeelezwa ukaguzi mwingine mkubwa wa vyeti unakuja ambao utatekelezwa kwa wauguzi ili kubaini wenye vyeti visivyokuwa halali. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Wanafunzi wa kike Wilayani Bagamoyo, Pwani wameaswa kuacha tamaa na kuepuka kuingia kwenye mtego wa mapenzi ya wanaume wadanganyifu. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Serikali imesema itatengeneza utaratibu wa kupima vinasaba (DNA) kwa wageni wanaoingia nchini ili kupunguza vifo. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Serikali imeanza kugawa viuadudu vya kutokomeza mbu kwa Halmashauri za mikoa 14 yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya malaria. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi amewataka WaTZ kushirikiana na Rais Magufuli katika kutunza rasilimali zilizopo nchini. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha hakuna mhalifu wa mauaji ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga ambaye atatoroka. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Sheikh Issa Nasoro ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuanza kutoa misamaha kwa wafungwa wakati wa sikukuu za dini #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Watoto 85 wamezaliwa usiku wa kuamkia Sikukuu ya Eid el Fitr katika Hospitali za Muhimbili, Temeke, Amana na Mnazi Mmoja DSM. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Kituo cha afya cha Kibakwe Mpwapwa kimesimamisha huduma ikiwemo ya upasuaji baada ya daktari kukumbwa ktk sakata la vyeti feki #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Waziri Mkuu Majaliwa amesema hakuna atakayechomoka Kibiti, Rufiji na kinachofanyika sasa ni kuchuja ili kupata wahalifu halisi #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Rais Shein amesisitiza kuwepo umakini katika kuandaa, kusimamia na kufuatilia mikataba ya mafuta na gesi ili kuepuka ubabaishaji. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Imeelezwa kuwa ndani ya miaka mitano ijayo ugonjwa wa malaria utakwisha endapo dawa za kuua mazalia ya mbu zitatumika vizuri #Tanzania DAIMA
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
TFDA imeteketeza bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu zilizoingizwa kwa njia za panya na kuuzwa kinyuma cha sheria. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye amelifananisha sakata la makinikia na mchakato wa Katiba Mpya kwa namna ulivyotumia fedha. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CHADEMA, Edward Lowassa anatakiwa na Polisi leo kwa ajili ya mahojiano. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana alifika nyumbani kwa mbunge wa zamani wa Moshi marehemu Philemon Ndesamburo kutoa ubani #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Viongozi wa Dini na Serikali wameitumia Sikukuu ya Eid el Fitr kulaani mauaji yanayeondelea Kibiti, Rufiji na Mkuranga. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Taasisi za Kiislamu Tanzania zimeitaka Serikali kutenda haki kwa viongozi wa dini ili kuendelea kulinda amani na utulivu. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
"Kama si katiba ningeshauri John Magufuli awe Rais wa kudumu, kwa kuwa tuna katiba basi hatuna budi kuifuata-Rais mstaafu, Mwinyi #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Watu 5 wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamevamia kijiji cha Inteka, Mpanda na kupora mali za wafanyabiashara zaidi ya Tsh. 4m. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Ole Sendeka, Ole Millya wataka kutwangana hadharani Simanjiro, ni baada ya kila mmoja kutamba kufanikisha maendeleo ya jimbo hilo #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema watu wanaofanya mauaji Pwani si Waislamu kama ambavyo baadhi ya wananchi wanahisi #NIPASHE
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Serikali imesema kuanzia sasa itataifisha mahindi na malori yote yatakayokamatwa yakivusha chakula kwa magendo kwenda nje ya nchi #NIPASHE
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda ameiomba Serikali kubadilisha jina la kijiji cha Zuzu ambacho anaishi, aomba kiitwe Zinje #NIPASHE pic.twitter.com/HzJtLlqwQb
— millardayo (@millardayo) June 27, 2017
Meya afunguka baada ya kibao cha Victor Wanyama kung’olewa!!!