Baada ya kusomwa kesi ya Rais wa Simba SC Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange Kaburu, iliyofuata kusomwa ilikuwa kesi ya Rais wa TFF Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wake Mwesigwa Selestine na Siande Mwanga chini ya Hakimu Wilbroad Mashauri.
Kesi hiyo ilichukua muda kidogo kufanyiwa maamuzi ya awali kutokana na mawakili pande za walalamikiwa na mlalamikaji kuvutana kwa vifungu kuhusiana na suala la dhamana baada ya Jamal Malinzi na wenzake wawili akiwemo Katibu Mkuu wake kutuhumiwa kwa kosa la utakatishaji fedha ambalo kisheria linawanyima dhamana.
Baada ya mawakili wa upande wa mlalamikaji kuomba kesi hiyo iahirishwe kwa madai ya upelelezi kutokamilika, mawakili wa upande wa mtuhumiwa ambaye ni Malinzi na wenzake waligomea kesi hiyo kuahirishwa wakidai kuwa kama upelelezi haujakamilika hawapaswi kwenda rumande.
Mvutano wa kisheria na kanuni ulitawala kwa muda mrefu ukifuatiliwa na Hakimu Wilbroad Mashauri kuamua kuahirisha kesi hadi Jumatatu July 3 kujua kama watapata dhamana au la.
Jumla ya mashitaka 28 wanatuhumiwa nayo Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Mwesigwa Selestine na mwanamke mmoja ambapo mashtaka 25 kati ya hayo yanamkabili Malinzi mengi yakihusu kughushi nyaraka za kuidai TFF kiasi tofauti tofauti cha fedha.
VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1