Leo June 29, 2017 Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ kupitia kwa Katibu wake wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole imekutana na Waandishia wa Habari katika mkutano uliofanyika katika Ofisi ndogo ya CCM Lumumba DSM.
Katika mkutano huo, CCM imezungumzia mambo saba ikiwemo kuunga mkono juhudi na kazi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ya CCM.
Polepole alisema:>>>”Chama cha Mapinduzi kinapenda kuchukua nafasi hii kuueleza umma wa Watanzania kwamba tunaridhishwa sana na kazi nzuri ambayo Serikali ya Awamu ya Tano ya Chama cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Rais Magufuli wanayoifanya.
Aidha, Polepole amegusia issue ya wanafunzi waliopata ujauzito kutorudi shuleni baada ya kujifungua akisema kuwa Chama hicho kinaunga mkono kauli ya Rais kwa asilimia zote ya kukataza wanafunzi wajawazito kutorudi shuleni baada ya kujifungua akisema jambo hilo ni sera.
“Chama cha Mapinduzi kinaunga mkono kwa asilimia zote ya Rais Magufuli ya kutokuruhusu watoto waliopata ujauzito kurudi katika mfumo rasmi wa elimu…Chama cha Mapinduzi kimekuwa kinafuatilia jambo hili na tumeona kuna watu wanataka kupotosha jambo hili…jambo hili kwenye Chama cha Mapinduzi ni jambo la kisera.” – Humphrey Polepole.
Kujua mengi zaidi kuhusu mambo hayo 7 waliyozungumza na CCM bonyeza PLAY kwenye hii VIDEO kutazama!!!
Tamko la CHADEMA mbele ya waandishi DSM!!!