Leo June 30, 2017 ni siku ya mwisho katika mwezi huu ambapo yapo mengi yaliyojiri tangu asubuhi hadi usiku ambapo unapata fursa ya kuyasikia mambo hayo kwenye Amplifaya ya Clouds FM kuanzia saa 1:00 Usiku hadi saa 3:00 Usiku na kama ulikosa kusikiliza Radio wakati huo nimekukusanyia story zote na kukusogezea.
#AmplifayaUPDATES "Unapowaona wenzako wengi namna hii, waliochaguliwa na watu halafu unawaona wao ni dhaifu lazima una matatizo"-Ndugai pic.twitter.com/VYlNQ7FZ62
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
#AmplifayaUPDATES "Mnakimbiakimbia mara kufungua madudu gani sijui? hakuna cha kesi, hapa mwaka mtu hakanyagi hapa, mimi ndio spika"-Ndugai pic.twitter.com/0umfDWll7f
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
#AmplifayaUPDATES Jengo jipya la uwanja wa ndege DSM litakapokamilika kwa mwaka litaweza kuhudumia abiria milioni sita pic.twitter.com/Upv9OOd7X6
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
#AmplifayaUPDATES 'Kwa kuwa miswada ya madini imekuja, wabunge waifanyie kazi badala ya kupoteza muda kujadili kuhusu muda"-@zittokabwe pic.twitter.com/WC8wnpRBLV
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
#AmplifayaUPDATES "Kuna kipindi nilikuwa nafanya huduma sehemu mbalimbali lakini sasa hivi nimeanzisha kanisa langu"-Pastor Myamba pic.twitter.com/l4ASvgM94U
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
#AmplifayaUPDATES Wananchi wametakiwa kutokuwa na wasiwasi kuhusu treni za umeme kwani hujengewa nyaya maalumu zinatofautiana na za kawaida
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
https://twitter.com/millardayo/status/880847764384624643
#AmplifayaUPDATES Unaambiwa kwa sasa watu binafsi hawataruhusiwa kuwa na treni binafsi kwani shirika la reli ndilo litakuwa msimamizi mkuu
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
#AmplifayaUPDATES Unaambiwa treni ya umeme haitasimama kama umeme wa TANESCO ukikatika ghafla
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
#AmplifayaUPDATES Nauli ya treni za umeme haitakuwa sawa na treni za kawaida kwani zinatumia teknolojia ya kisasa hivyo nauli itakuwa juu
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
#AmplifayaUPDATES Treni ya umeme itakuwa na uwezo wa kusafirisha wagonjwa mahututi, ina mwendo wa haraka na itatumia Dakika 90 Moro-DSM pic.twitter.com/D25jt152ex
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
https://twitter.com/millardayo/status/880841834477625345
#AmplifayaUPDATES Mradi wa treni za umeme ukikamilika, treni zitakuwa zinasimama kwenye vituo sita kutokea DSM -Morogoro pic.twitter.com/EH1o4uvPgE
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
#AmplifayaUPDATES Leo kimezinduliwa rasmi kituo cha mabasi kikubwa Singida ambacho kimegharimu zaidi bilioni 3
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
#AmplifayaUPDATES Msanii kutoka Uganda, Bob Wine ameshinda ubunge, alikuwa anagombea kama mgombea huru kwenye uchaguzi nchini Uganda pic.twitter.com/JPmBllGh8m
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
#AmplifayaUPDATES Kuanzia kesho bei za jumla na rejareja za mafuta ya Petroli, Dizeli na mafuta ya taa zimepungua kwa Tsh 37 kwa lita pic.twitter.com/bkcQ2QGhBx
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Waziri Mwalimu kuhusu wanafunzi waliojifungua kurudi shule!!!!