Wakati headlines za hatma ya Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa zikiendelea kutawala wakiwa chini ya mikono ya sheria kwa tuhuma mbalimbali, headlines mpya zimeibuka kuhusiana uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo.
Uchaguzi Mkuu wa TFF ulipangwa kufanyika August 12 2017 lakini mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Revocatus Kuuli ameamua kuahirisha kutokana na sababu kuu ikitajwa kuwa uwepo wa mgawanyiko ndani ya kamati hiyo, hivyo leo July 2 Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Salum Madadi amepokea taarifa za kuahirishwa kwa uchaguzi Mkuu.
“Tuna neno moja tu ambalo tunataka liwafikie wadau wetu wa mpira hapa nchini, kumejitokeza mgawanyiko kwenye kamati yetu ya uchaguzi katika kipindi hiki cha mchakato wa uchaguzi na tumepokea barua ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi tumeshauriana nae na tumesitisha zoezi la mchakato wa uchaguzi” >>> Salum Madadi
Miongoni mwa vitu vinavyodaiwa kuleta tofauti ni kukosekana wakati wa usaili kwa mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya Urais Jamal Malinzi anayetetea nafasi yake na Geofrey Nyange Kaburu anayegombea nafasi ya Makamu wa Rais, Kaburu na Malinzi wote wapo rumande kwa tuhuma tofauti.
VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1