Kutokana na kuwepo kwa matukio ya nyumba za watu kuungua moto Jeshi la Polisi Kagera limewakamata watu wawili wanaosadikiwa kuchoma moto nyumba za watu katika kijiji cha Bugasha kilichopo Kata ya Mayondwe, Muleba..
Kamanda wa Polisi Kagera Augustine Ollomi amesema kuwa July 2 mwaka huu ilichomwa moto nyumba nyingine ya mzee wa miaka 60 na kufikisha jumla ya nyumba 14 tangu zimeanza kuchomwa mpaka sasa.
Kamanda Ollom amewataja waliokamatwa kuwa ni Badiru Daniel miaka 32 aliyejitambulisha kuwa ni Mshubi lakini Jeshi la Polisi limembaini kuwa ni Mrundi, na wa pili ni Angela Karisti miaka 36 Mhaya mkazi wa kijiji Bisole kata mhutwe ndani ya wilaya hiyo.
Polisi wamesema hadi sasa tayari wameshamjua mhusika mkuu wa matukio hayo ambaye anafahamika kwa jina la Shakiru Mohammed miaka 42 mkazi wa kijiji Bugasha. Unaweza kuendelea kumsikiliza kamanda wa Polisi Kagera kwenye hii video hapa chini…
VIDEO: Mbunge Musukuma kuhusu wanaoikosoa Serikali