Tayari nimekukusanyia uchambuzi wa stori zote kubwa za magazeti ya Tanzania leo July 6, 2017 ambapo kila siku huwa nazipandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Serikali imeombwa kuimarisha ulinzi katika eneo linalotarajiwa kuwekwa miundombinu ya mradi wa bomba la mafuta ghafi. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Mahakama ya Wilaya ya TMK imemhukumu kifungo cha mwaka 1 jela Diwani wa Viti Maalumu Mwanakombo Ramadhan (CCM) kwa kutishia kuua. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
"Watanzania hatujazoea vurugu namna hii kama wametumwa, wametumwa vibaya." – IGP Sirro. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Edna Deusi (21) anashikiliwa na Polisi Mwanza kwa kumng'ata ulimi shangazi yake aliyemfokea baada ya kujikojolea kitandani. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Serikali imesema haina mpango wa kuanzisha maeneo mapya ya utawala hadi iboreshe miundombinu kwenye maeneo iliyoyaanzisha. #MTANZNIA.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge Tundu Lissu na Wahariri wa gazeti la Mawio imeahirishwa hadi August 7 mwaka huu. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Wabunge wa Upinzani wameendelea kukilaumu kiti cha Spika kuendesha shughuli kwa kuangalia uchama badala ya maslahi ya Taifa. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
IGP Sirro amesema muda si mrefu majibu ya mauaji ya raia yanayoendelea ktk Wilaya za Ikwiriri na Kibiti, Pwani yatapatikana. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Mmiliki wa Lucky Vincent anayedaiwa kuruhusu gari lake kubeba abiria bila leseni na bima, atasomewa maelezo ya awali July 26. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
BAVICHA imelalamikia kufinywa demokrasia na uhuru wa habari wakihoji sababu za vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Imeelezwa kuwa miezi 4 iliyopita Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata watuhumiwa 4,809 na kufungua kesi 3,222, #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Wakili mwandamizi wa kujitegemea Jerome Msemwa amejitoa kumtetea Rais wa TFF, Malinzi na wenzake wanaotuhumiwa kutakatisha fedha. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Spika wa Bunge Job Ndugai ameunda Kamati Maalum ya ushauri kuhusu mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa Almasi. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu DSM linaendelea kumshikilia na kumhoji Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa amri ya DC wa Kinondoni. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Madiwani 18 kati ya 21 wa CUF DSM wameungana na Wabunge 40 kumpinga Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili, Prof. Ibrahim Lipumba. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
IGP Sirro amewataka wananchi Pwani kujilinda kupitia vikundi vya ulinzi shirikishi na kushirikisha Polisi kukabiliana na mauaji. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Wakuu wa Wilaya wametakiwa kusimamia utekelezaji wa sheria za nchi zenye lengo la kumlinda mtoto wa kike dhidi ya mimba shuleni. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Serikali imeshauri wafanyabiashara na watu wanaokusudia kwenda Mashariki mwa DRC kuwa waangalifu kutokana na kutekwa madereva. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Serikali imesema mikataba ya madini iliyopo ni ya mwisho hivyo wawekezaji watakaokuja kuwekeza kuanzia sasa watatumia leseni. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Mahakama ya Rufani imekubali rufani ya Jamhuri kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi haina mamlaka kusikiliza maombi ya mawakili wa UAMSHO. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Serikali itawapa mafunzo ya mtaala ulioboreshwa walimu 600 wa Shule za Msingi wanaofundisha Darasa la 3&4 July 10-30 mwaka huu. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
M/kiti wa Kitongoji cha Londo, Kibiti Michael Martin (28) yuko hatarini kutoona baada ya kufanyiwa upasuaji kutolewa jicho la kulia. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilihamia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili kumsomea mashtaka 7 Yusuf Manji akiwa amelazwa. #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Serikali imesema madereva 21 wa Tanzania waliotekwa na kikundi cha waasi cha Mai-Mai nchini DRC bado wapo kwenye msitu wa Lulimba. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Bunge limeagiza Mbunge Halima Mdee kuitwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kwa utovu wa nidhamu. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Bodi ya maziwa Tanzania (TDB) imewataka wauzaji wadogo wa maziwa kuunda vikundi ili kurahisisha uzambazaji wa hiyo. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 6, 2017
Kilichoendelea baada ya Mahakama kuhamia Hospitali kumsomea mashtaka Manji!!!