Kama kawaida millardayo.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku kupitia twitter account @millardayo na leo July 9, 2017 pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali ya Tanzania.
Chukua muda wako kupitia kila udondozi wa kilichoandikwa kwenye magazeti hayo.
Mwendesha bodaboda mkazi wa Sirari, Tarime mkoani Mara, Makerere Sorai (24) ameuawa na majambazi na mwili wake kutupwa mtaroni. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Serikali Mbarali imetoa siku 3 wafugaji, wakulima wa Imalilo Songwe na Luhanga waondoe mazizi pembeni mwa Mto Ruaha na Mbarali. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Wakulima wa Madaba, Ruvuma wametakiwa kuacha kupulizia kemikali za sumu kwenye vyanzo vya maji ili kuzuia magugu na nyasi kuota. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Watanzania wametakiwa kutumia korosho zinazozalishwa nchini kwa kuwa bidhaa hiyo ni muhimu sana katika kulinda afya. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Serikali Mkoa wa Rukwa imewatoa hofu viongozi na wageni wanaosita kutembelea Mkoa huo kwa kuwa sifa ya uchawi haipo tena. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Dhamira ya Serikali kuunganisha mikoa yote na umeme inaendelea vizuri kutokana na miradi kadhaa ya kuzalisha umeme kuimarika . #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Serikali imewahakikishia wafanyabiashara kuwa Tanzania itabaki kwenye soko la Ukuzaji Fursa ya Kiuchumi Afrika (AGOA). #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Serikali inaandaa utaratibu wa kuwa na maghala kwenye mikoa yote inayolima zao la korosho kwa ajili ya ukusanyaji wa zao hilo. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Naibu Waziri wa Mazingira amesema Serikali imejipanga kuondoa kero za upatikanaji wa vyeti vya tathmini ya athari za mazingira. #MZALENDO.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Imeelezwa kuwa baada ya Yusuf Manji kuondolewa Hospitali na kupelekwa Keko, kumekuwa na taarifa zenye utata kuhusu afya yake. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Wakati Polisi DSM ikiendelea kumshikilia Mbunge Halima Mdee (CHADEMA), Chama hicho kimepanga kumfikisha DC Hapi Mahakamani. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
ACT-Wazalendo imewataka Wakuu wa Mkoa na Wilaya kufuata Sheria ikidai wanatumia sheria ya kuwakamata wapinzani kinyume. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Vijana wameakiwa kujitambua na kuacha mipango ya kuwaingiza kwenye uhalifu unaoweza kuvuruga maono yao na kuwakwamisha kimaisha. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Mahakama ya Wilaya ya Maswa, Simiyu imemhukumu Njana Hame miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka na kumsababishia mimba mwanafunzi. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Mkazi mmoja wa Nyambwanda, kijiji cha Hanga, Kibiti anayetambulika kama Juma Ndikanye ameuawa kwa risasi usiku wa kuamkia jana. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Polisi Mwanza imedai kuwauwa watu 6 wanaodhaniwa kuhusika na uhalifu wa kutumia silaha unaoendelea Kibiti na Rufiji, Pwani. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Zaidi ya wanafunzi 10 wa Shule za Sekondari Wilayani Njombe wamedaiwa kushindwa kuendelea na masomo baada ya kupata ujauzito. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
UVCCM imewashauri wahitimu Vyuo Vikuu kuzitumia fani na elimu zao katika utafiti wa kitaaluma kulingana na changamoto zilizopo. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Kufuatia Polisi kumshikilia kwa zaidi ya saa 48 Halima Mdee, DC Ally Hapi aliyetoa agizo la kukamatwa kwake amejivua sakata hilo. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 9, 2017
Mtanzania aliyekataa mshahara wa Tsh. Milioni 425 Marekani amerejea nyumbani!!!