Nahodha wa zamani wa Everton ambaye kwa sasa ni moja kati ya watu wenye heshima kubwa katika club hiyo Leon Osman aliwasili Dar es Salaam Tanzania jana akiwa tayari kwa kuelekea kutalii mbugani Arusha lakini alikutana na waandishi wa habari.
Leon Osman ambaye ni sehemu ya msafar wa timu ya Everton unaokuja Tanzania kucheza na Mabingwa wa SportPesa Super Cup Gor Mahia ya Kenya uwanja wa Taifa Dar es Salaam aliongea na waandishi wa habari baada ya kuwasili Dar es Salaam na kueleza kuwa game itakuwa na ushindani na haichukulii poa.
“Bila shaka mechi hiyo itakuwa na mvuto kuitazama kwa sababu Gor Mahia wamefanya kazi nzuri kwa kutwaa ubingwa wa SportPesa Super Cup ili waweze kucheza mechi na Everton ni fursa nzuri lakini bado nina imani kuwa Everton watashinda mechi, kwani Everton wamekuwa wakijifua kwa wiki nzima sasa”
Msafara wa awamu ya pili pamoja na timu ya Everton watawasili July 12 ikiwa ni siku moja kabla ya mechi hiyo itakayochezwa uwanja wa Taifa, kiingilio cha kuona game hiyo ya kihistoria ni Tsh 3000 mzunguuko na kwa VIP C Tsh 8000, Everton inakuja Tanzania na kikosi chake cha kwanza.
VIDEO: Taifa Stars ilivyopokelewa, Kocha Mayanga kathibitisha wamemuacha mchezaji South